Gabriel Jesus ameanza rasmi maisha yake ya soka ndani ya Ulaya baada ya kwenda England kwa mara ya pili baada ya kupumzika muda wa sikukuu na familia yake. Jesus amefika Manchester na mama yake pamoja na mdogo wake.
Wamepokelewa na hali ya hewa ya baridi kali akitokea Brazil ambapo aliisaidia club yake ya toka utotoni kutwaa taji baada ya miaka 22. Kiasi cha pound milioni 27 kilicholipwa kumpata Jesus kinatakiwa kuonekana kwenye mechi za hivi karibuni.
Man City wamepitia mechi kadhaa na kupoteza kitu ambacho kinawarudisha nyuma kwenye mbio za kuchukua makombe hasa ubingwa wa EPL. Swali ni kwamba Gabriel Jesus atasaidi kuiweka Manchester City kwenye nafasi nzuri kwam muda huu au itamchukua muda mrefu zaidi kuzoea ligi maarufu ya England.
Hizi ni picha alivyowasili…
No comments:
Post a Comment