Wednesday, 4 January 2017

Bill na Hillary Clinton kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Trump

Bill Clinton na mke wake Hillary wamepanga kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Donald Trump, kwa mujibu wa ripoti.

Familia hiyo itahudhuria sherehe hizo jijini Washington, D.C. January 20 kumwangalia Trump akiapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.

Pia Rais wa zamani wa nchi hiyo, George W. Bush ametangaza kuwa atahudhuria sherehe hizo pamoja na mke wake, Laura. Hata hivyo taarifa ya Bush imedai kuwa baba yake, George H.W., hatohudhuria kutokana na umri wake kuwa umeenda sana.

MAAMUZI mapya ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu mauaji ya wakulima na wafugaji


January 3, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amefika katika kijiji cha Tindiga kilichopo wilaya ya Mikumi zilipotokea vurugu zilizopelekea mkulima mmoja kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni na kusikiliza kero zinazowasumbua wananchi wa Kilosa kabla ya kutoa maamuzi. 

Waziri Mwigulu amesema kuanzia sasa likitokea tukio lolote la watu kuuana kwa mapanga, mikuki, sime  na silaha zozote za jadi zinazotumiwa hasa na wakulima na wafugaji, serikali itafuta utaratibu wa kubeba silaha hizo na atakayebeba atakamatwa na kuchukuliwa hatua kama watuhumiwa wengine.

Kinginie alichoagiza Waziri Mwigulu ni wakuliam na wafugaji kwa pamoja kuwakamata watu wote watakaohusika na kuanzisha vurugu na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola kabla jeshi la polisi halijafanya maamuzi yake.

“Kuanzia leo tunaanza kuhesabu pakitokea tukio lolote la vurugu na zikatumika silaha kuwadhuru wananchi, tutafuta utaratibu wa watu kutembea na silaha mitaani, na ukikutwa nayo unakamatwa kama ambavyo mtu mtu mwenye silaha ya moto na hajaiandikisha. Hatuwezi kuruhusu hii ikawa nchi ya watu wanakatanakatana tu” – Waziri Mwigulu Nchemba

Tuesday, 3 January 2017

Afcon 2017: Mohammad Salah Joins Egypt Camp

As the kickoff of the 2017 African cup of Nations draws nearer, several teams are in final preparations with many players joining team camps.

Egypt’s star Mohammad Salah joined Hector Cupper’s camp in training on Tuesday after arriving from Italy where he plies his trade at Serie A side AS Roma.

Salah who had an ankle injury concern at the start of last month that saw him sit out for three weeks has recovered in time ahead the African cup of Nations championship.

The Egyptian winger joined teammates in training in Cairo on Tuesday as they prepared for a friendly game against Tunisia on 8th January.

The other player who joined the Pharaohs in Tuesday training is Stoke City winger Ramadan Sobhi.

Only two players are yet to join Hector Cupper’s camp with Hull City’s Mohammad El Mohamady and Arsenal’s Mohammad Elneny with the latter performing Umrrah in Mecca, Saudi Arabia.

The duo is set to join the rest of the team on Wednesday.

Egypt are in group D alongside Uganda, Mali and Ghana and kick start their campaign on 17th January against Mali.

Egypt provisional squad

Goalkeepers: Ahmed El-Shennawy, Essam El- Hadary, Sherif Ekramy, Mohamed Awad.

Defenders: Ahmed Fathi, Ahmed Elmohamady, Mohamed Abdel-Shafy, Karim Hafez, Hamada Tolba, Ahmed Hegazy, Saad Samir, Ahmed Dweidar, Ali Gabr, Omar Gaber.

Midfielders: Mohamed Elneny, Tarek Hamed, Ibrahim Salah, Abdallah El-Said, Amr Warda, Ramadan Sobhi, Mohamed Ibrahim, Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’.

Forwards: Ahmed Hassan ‘Koka’, Ahmed Gomaa, Marwan Mohsen, Mahmoud Abdel-Moneim ‘Kahraba’, Mohamed Salah

Aina tatu za posho zilizofutwa na serikali katika halmashauri zote nchini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wialaya ya Kigamboni Januari 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wialya ya Kigamboni baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Ametia agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

“Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.

Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,”amesisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Pia amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
2 MTAA WA MAGOGONI, 
S. L. P. 3021, 
JUMANNE, JANUARI 3, 2017

POLISI kufukua kaburi la binti aliyezikwa kwa siri Arusha


Familia moja  jijini Arusha inadaiwa kumzika kwa siri mtoto wao mdogo wa kike wa miaka mitatu katika kaburi lililofichwa, huku majirani wakidanganywa kuwa binti huyo yupo hai.

Taarifa za kisa hicho cha kusikitisha zimevifikia vyombo vya usalama. Kwa sasa kuna mipango ya kuhakikisha kuwa mwili wa binti huyo, Nuru Losipha aliyezikwa kwa siri na familia yake, unafukuliwa kwa uchunguzi zaidi.

Inadaiwa kuwa Losipha alipoteza maisha wakati akifanyiwa tohara au ukeketaji na ngariba, ambaye jina lake halikufahamika mara moja, huku familia yake ikishuhudia.

Kitendo hicho kilifanyika katika kijiji cha Engutoto Kata ya Mwandeti wilayani Arumeru Desemba 28, mwaka jana, zikiwa zimebaki takriban siku tatu tu, kabla ya mtoto huyo aliyekuwa na umri wa miaka mitatu tu, hajaingia mwaka mpya wa 2017.

Mtendaji wa Kata ya Mwandeti, Njivaini Kivuyo awali alikuwa amepitwa na taarifa hizo hadi vyombo vya habari vilipotinga kijijini hapo kwa uchunguzi na ndipo alipolazimika kwenda kuripoti tukio hilo kwenye kituo cha Polisi cha Ngaramtoni.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo aliapa kuwa liwalo na liwe na kwamba ikiwezekana kaburi litafukuliwa ili mwili wa malaika huyo asiye na hatia, uchunguzwe upya.

“Ndio kwanza nazipata hizi taarifa, na kama polisi tutaomba kibali cha mahakama ili twende kulifukua kaburi husika tujiridhishe kama kweli mtoto huyo amezikwa humo na iwapo tutaukuta huo mwili, basi tutaanza uchunguzi juu ya kifo chake,” alisema Kamanda arles Mkumbo.

Baba wa marehemu, Losipha Kaiser anadai kuwa mtoto wake alifariki kutokana na ugonjwa wa baridi yabisi na kwamba aliugua kwa kipindi kirefu kabla ya kupoteza maisha Desemba 28, mwaka jana. Lakini madai yake hayo yanapingana na ripoti ya muuguzi katika duka la dawa lililopo kijiji cha jirani cha Kidali, anayeitwa Jane Andrew.

“Walimleta mtoto hapa walitaka nimsaidie tiba, lakini tayari huyo binti alikuwa amezimia na kutokwa na damu nyingi,”alidai.

Muuguzi huyo aliwahimiza wamkimbize mtoto hospitali, na hakufahamu nini kiliendelea hadi ripoti za kifo zilipomfikia.

Huku serikali ikipiga marufuku vitendo vya ukeketaji kwa wasichana, bado kuna familia nyingi kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa, zinaendeleza mila hiyo kwa siri.

Kwa sasa familia hizo zimegundua mbinu mpya ya kuwatahiri watoto wa kike wakiwa wadogo sana, kuepuka kukamatwa.

Ngariba wanaotumika kukeketa watoto, mara nyingi ni akina mama vikongwe wasiokuwa na ujuzi, taaluma za afya na hutumia vifaa butu, ambazo husababisha uvujaji mwingi wa damu na kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa mengine.

All The Trending Images This Wednesday

The Christmas mood is slowly disappearing and the reality of ‘Njaanuary’ settling in. As usual, we start the day with a collection of the trending memes, images and tweets. 


Mlinzi mwingine auawa Geita....Aliyepigwa na wafugaji Morogoro Afariki Dunia

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi
 Mauaji ya walinzi mkoani Geita yamendelea kuwa tishio kwa usalama wao baada ya mlinzi mwingine aliyekuwa akilinda maduka yapatayo 15, kuuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani. 

Mauaji ya mlinzi huyo Kisusi Iddy (40) aliyekuwa akilinda maduka hayo kwenye Mtaa wa Mwatulole, ni muendelezo wa matukio ya kuuawa walinzi wa maduka na mali mbalimbali kwani katika kipindi cha miaka miwili  jumla ya walinzi 20 wameuawa. 

Taarifa zilizopatikana jana kuhusu mauaji ya mlinzi huyo na kuthibitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo, Fikiri Toi zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Januari Mosi na wauaji hao hawakuiba kitu chochote. 

Mwili wa Iddy ulikutwa umefunikwa kwa shuka lake alilokuwa akilitumia lindoni, huku likiwa limetapakaa damu. 

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amefuta vibali vyote vya waganga wa tiba za asili kwa madai wao ni moja ya chanzo cha imani za kishirikina zinazosababisha mauaji hayo.

 Alisema kutokana na kukithiri kwa mauaji hayo, mamlaka yake inakusudia kufufua Jeshi la Jadi (Sungusungu) ili kusaidia kuyadhibiti. 

Hata hivyo, Kapufi alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa wakati wa uhai wake, Iddy alikuwa analinda maduka ya wafanyabiashara yanayofikia 15 na kwamba baada ya kufuatilia, hakuwa na mafunzo yoyote ya ulinzi.

 Aliyepigwa na wafugaji Moro afariki 

Fabian Bago (21) anayedaiwa kushambuliwa na wafugaji katika Kijiji cha Kolelo, Morogoro, amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Frank Jacob alisema kijana huyo alifariki dunia saa 11 jioni jana akiwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu na kwamba mwili wake umehifadhiwa kusubiri taratibu nyingine za kipolisi.

 Dk Jacob alisema mara baada ya kufikishwa hospitalini hapo, kijana huyo alifanyiwa vipimo na matibabu lakini alifariki dunia kutokana na majeraha makubwa kichwani yaliyoharibu sehemu ya ubongo. 

Baba mzazi wa kijana huyo, Alan Bago alisema ameshatoa taarifa polisi kuhusina na kifo cha kijana wake na sasa anasubiri maelekezo ya polisi ili aweze kuendelea na taratibu za mazishi.